Rais Samia aridhia nyongeza ya mishahara kwa asilimia 23.3

Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia mapendekezo ya kuongeza mishahara ikiwemo kima cha chini kwa watumishi wa umma kwa asilimia 23.3, ambapo Sh1.59 trilioni itatumika kwa ongezeko hilo. Taarifa iliyotolewa leo Mei 14 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus inasema mapendekezo hayo ni mwendelezo wa kikao cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alichokifanya hivi